MAFUSHO YA KILA NYOTA
PUNDA (QIST)
Mafusho haya yako kama vijiti, yana rangi ya
kahawia ni kwa wenye nyota ya Punda, siku yao ni Jumanne, unachoma kati ya saa
12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
NG’OMBE (MUSTAKA)
Mafusho haya yako kama vijiwe vidogo vidogo vyenye vumbi na vina rangi ya
kijivu jivu na ni kwa wenye nyota ya Ng’ombe,
siku yao ni Ijumaa unachoma kati
ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
MAPACHA
(KACHIRI)
Mafusho haya yako kama mauwa yaliyo kauka na rangi yake ni kahawia na ni ya
wenye nyota za Mapacha, siku yao ni Jumatano choma kati ya saa 12-1 asubuhi au
kati ya saa7-8 mchana.
KAA (UBANI)
Hapa unaweza kutumia ubani wa aina yeyote
wakawaida au ubani maka unachoma siku ya Jumatatu kati ya saa 12-1 asubuhi na saa7-8
mchana. Nyota yake ni Kaa (CANCER)
(SIMBA) (SANDARUS)
Mafusho haya yako kama mawe yenye rangi ya njano ni kwa wenye nyota ya
Simba (Leo) ambao siku yao ni Jumapili, unachoma katika muda wa Shams ambao ni
kati ya saa12 asubuhi na saa moja asubuhi au saa saba mpaka saa nane mchana
MASHUKE (KACHIRI)
Mafusho haya yako kama mauwa yaliyo kauka na rangi yake ni kahawia na ni ya
wenye nyota ya mashuke, siku yao ni Jumatano choma kati ya saa 12-1 asubuhi au
kati ya saa7-8 mchana
MIZANI MUSTAKA
Mafusho haya yako kama vijiwe vidogo vidogo vyenye vumbi na vina rangi ya
kijivu jivu na ni kwa wenye nyota ya Mizani, siku yao ni Ijumaa unachoma kati
ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
NGE(QIST)
Mafusho haya yako kama vijiti, yana rangi ya kahawia ni kwa wenye nyota ya
Nge, siku yao ni Jumanne, unachoma kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
MSHALE- UDI-KAFURU
Hapa unaweza kutumia udi wa aina yeyote ambao unachanganya na kafur. Hii
kafur ina rangi nyeupe na mafusho haya ni kwa wenye nyota ya Mashale, siku yao
ni Alhamisi unachoma kati ya saa 12-1 asubuhi au saa 7-8 mchana.
MBUZI MIATUN –
SAILA
Mafusho haya yako kama lami nyeusi, yana mafuta
mafuta na yana harufu kama mvuje ni kwa wenye nyota ya Mbuzi, siku yao ni
Jumamosi unachoma kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana
NDOO MIATUN – SAILA
Mafusho haya yako kama lami nyeusi, yana mafuta mafuta na yana harufu kama
mvuje ni kwa wenye nyota ya Ndoo. siku yao ni Jumamosi unachoma kati ya saa
12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
SAMAKI UDI-KAFURU
Hapa unaweza kutumia udi wa aina yeyote ambao unachanganya na kafur. Hii
kafur ina rangi nyeupe na mafusho haya ni kwa wenye nyota ya Samaki, siku yao
ni Alhamisi unachoma kati ya saa 12-1 asubuhi au saa 7-8 mchana.
UCHAWI WA MAFUSHO
Unaweza ukatumia mafusho katika kufanya watu wapendane au watengane.
Kupendana kwa maana mapenzi yaendelee kuwepo au ndoa ishamiri na kutengana kwa
maana ya kuvunja ndoa au kufarakanisha
walo pamoja
MAPENZI
Ukitaka watu wapendane unatumia mafusho yafuatayo:
Ambar na udi, Rawandi, Kafur,
Zafarani na Mustaka. Mchanganyiko huu unachoma katika siku za Alhamis au Ijumaa au Jumatatu
kwa kutia nia ya jambo la mapenzi ulitakalo au unaweza kuchoma siku yoyote
katika saa za Atlarid, Zuhura au Qamar.
KUGOMBANISHA
Ukitaka kugombanisha unatumia mafusho yafuatayo:
Sandal nyekundu, Halititi,washqu (watu) na Miatun saila
Unachoma mafusho hayo siku ya Jumamosi au Jumanne au siku yeyote katika saa
za Zohal au Mariikh kwa kutia nia ya kutaka hao unaowataka
wagombane au kufarakana.
Labels:
nyota
No comments: