NJIA KUU YA KABALA YA KUITA MAJINI KWA HARAKA NA URAHISI ZAIDI
NJIA
KUU YA KABALA YA KUITA MAJINI KWA HARAKA NA URAHISI ZAIDI
NA
KUPATA CHOCHOTE UKITAKACHO KUTOKA KWA JINI
Kama jinsi ilivyokuwa kwa Masharti ambayo
yameshaelezwa hapo kabla juu ya kujitakasa na mengineyo; namna ya kumuita Jini
Mwenye Nguvu za Ajabu Kwa kutumia Njia Kuu ya KABALA ni kama ifuatavyo:-
Kwanza kabisa unatakiwa uwe na nia thabiti na ya
kweli, uwe Msafi pamoja na mambo mengine kwani usipokuwa hivyo utakapomuita
badala ya wewe kuwa na nguvu kubwa za kumdhibiti huyo Jini, yeye ndie ataweza kukudhibiti
kwa kuwa hukufuata maelekezo ya kujitakasa kwanza.
Iwapo utaelewa hayo; basi yaliyobaki ni rahisi
sana:-
Unatakiwa umpate Kuku Mweusi ambae hajawahi kamwe
kupandwa na Jogoo. Na unapomkamata uhakikishe ya kuwa hapigi kelele (halii kwa
sauti kubwa); hivyo ni bora zaidi kama utaweza kumkamata akiwa kwenye usingizi,
huku ukimkamata shingo yake ila usitumie nguvu za ziada sana katika kumzuia
asipige kelele.
Baada ya hapo unatakiwa uende moja kwa moja hadi
njia kuu na utembee hadi hapo utakapoikuta NJIA PANDA. Ukifika hapo subiri na
mara itakapofika Usiku wa manane (Saa Sita Kamili usiku), itapofika saa
hiyo unatakiwa Uchore Duara kwa kutumia Fimbo ya Mti wa Mvinje.
Baada ya Kuchora Duara hilo, unatakiwa uingie
katikati ya Duara hilo ulilolichora, na Unatakiwa Umgawanye Kuku huyo katika Vipande
viwili vinavyolingana na wakati ukifanya hivyo unatakiwa uwe unasema maneno
haya mara TATU (3) :..
“ELOIM,
ESSAIM, FRUGATIVI ET APPELLAVI”.
Baada ya kusema hayo, Geukia Upande wa
Mashariki, Piga magoti alafu sema Sala yako alafu malizia kwa kulitaja Jina
lake; ambalo ni ...“ROFOCALE”.
Wakati huo Jini atakutokea;
· Akiwa amevalia Koti refu lililodariziwa, lenye Rangi nyekundu,
· Fulana ya ndani ya Rangi ya Njano,
· Suruali yenye rangi ya Kijani isiyokolea.
· Kichwa chake kitakuwa kinafanana na kile cha Mbwa,
· Lakini Masikio yake yatakuwa yanafana na yale ya Punda,
· Kichwani atakuwa na Mapembe mawili,
· Atakuwa na Miguu na Kwato zinazofanana na za Ndama.
Atakuambia umuamrishe unalolihitaji akufanyie,
ambapo na wewe unatakiwa useme yale yote ambayo unayataka kwa kadri
itakavyokupendeza wewe mwenyewe.
Na kwa sababu ukiwa ndani ya hilo Duara
ulilolichora, HAWEZI kukudhuru na hatakuwa na njia nyingine ya kufanya
ila kufanya chochote kile utakachomuagiza, basi ujue ya kuwa utafanikiwa kupata
mambo mengi yote utakayoyaagiza na utafanikiwa kuwa Tajiri PAPO HAPO, na
utapata mafanikio na furaha kubwa Maishani mwako.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteSasa huyo kuku unamchinjia wapi he akuna njia nyingine endapo umemkosa huyo kuku mweusi
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteHakuna njia nyingine zaid ya SAA sita njia panda.
ReplyDeletehttp://wizardforums.com/Thread-The-Black-Hen ume-copy na ku-paste ila umebadir lugha
ReplyDelete