Vipindi za kila siku

[habari][bleft]

MAWE

[mawe][bleft]

NYOTA

[nyota][twocolumns]

videos

[videos][bleft]

MAJINI

[majini][twocolumns]

About Me

My photo
I am an Astrologer, Politician,,Jounalist by proffession,very much interested in current affairs and political news around the world.

VITU VINAVYOHITAJIKA WAKATI WA KUWAITA MAJINI


VITU VINAVYOHITAJIKA
WAKATI WA KUWAITA MAJINI:
MAANDALIZI.

Kwa mwenye kutaka kumuita Jini na kumtumia ahakikishe anazingatia mambo ya muhimu katika kutayarisha na kutafuta vifaa muhimu kwa ajili ya shughuli za kumuita jini.


Unatakiwa uwe na vifaa vifuatavyo

1.     Fimbo maalum
2.     Unyoya wa kwenye Bawa la kulia la Bata Mzinga
3.     Kitambaa safi cha hariri
4.     Mafusho
5.     Njiwa (damu ya njiwa)

FIMBO MAALUM:


Fimbo maalum ni kifaa cha kwanza ambacho kina umuhimu wa kipekee katika shughuli ya kuita Jini.

Hii fimbo maalum ni lazima itayarishwe katika siku na saa maalum na ni lazima itayarishwe kulingana na maelezo yake.

Pamoja na kazi nyingine muhimu ilizokuwa nazo hii fimbo maalum, pia inatumika wakati wa kuchora duara la kumuitia Jini pamoja na kumlazimisha afanye kama jinsi utakavyo wewe mwenyewe.

Fimbo katika shughuli hii ina maana na SIRI kubwa sana, na inatakiwa kutayarishwa kisahihi ili iweze kufanya kazi yake inayotakiwa.

Fimbo hii maalum kwa kawaida inaweza ikatengenezwa kutokana na miti ifuatayo;

1.     Mvinje.
2.     Henzirani au Ufito wa Mwanzi.
3.     Mti wa aina ya Hazel.

Fimbo hizi zinazotokana na hii miti zinatakiwa zote ziwe bado changa, yaani ambazo hazina matawi mengi.

Itakuwa ni vizuri zaidi iwapo utapata mti ambao una umri wa kama miezi 6.

Unatakiwa utafute mti wa mvinje au fito ya mwanzi.

Unatakiwa uangalie mti ambao hauna matawi au haujatoa machipukizi mengi na iwapo utapata ambao bado ni mchanga itakuwa ndio vizuri zaidi.

Iwapo utakuwa umechagua mti unaojulikana kama “hazel” basi unatakiwa uupate ambao kamwe haujatoa matunda na unatakiwa uangalie tawi ambalo linaweza kutoa fimbo ya saizi ya inchi kumi na tisa na nusu (19 ½) .

Baada ya kuuona huo mti:

Baada ya kuuona huo mti utakaofaa unatakiwa usiushike wala kuugusa ila uuangalie tu, rudi nyumbani na usubiri hadi kesho ambayo inatakiwa iwe siku ya Jumapili asubuhi.

Siku ya Jumapili asubuhi na mapema wakati jua linachomoza unatakiwa uukate huo mti kwa kisu ambacho bado hakijatumika (kipya).

Unatakiwa uukate kwa pigo moja tu na mara baada ya kuukata huo mti unatakiwa uuondoe matawi yote ambayo utakuwa nayo.

Baada ya kuondoa matawi na kuitengeneza vizuri hiyo fimbo unatakiwa huku ukiwa umegeukia upande ambao jua linachomoza (upande wa Mashariki);

Useme maneno yafuatayo:

“Kwa nguvu za ADONAI Mkuu ninaiamuru hii fimbo iweze kufanya kazi ambazo mimi ninataka inifanyie bila ya kupungua uwezo wowote ule. Iwe na nguvu kubwa za kunilinda na kuvuta kwangu na kunifanikisha kile ninachotaka kukifanya kwa amri za nguvu za radi za Mkuu Zariatnatmik”

Baada ya kusema maneno hayo huku ukiwa bado unaangalia upande wa Mashariki, unaweza kuendelea kuimalizia kuitengeneza vizuri hiyo fimbo.

Baada ya kumaliza kuikata na kuitengeneza hiyo fimbo mnamo siku hiyo ya Jumapili, ichukue na uhifadhi katika kitambaa cha Hariri.

Baada ya hapo ichukue ukaihifadhi nyumbani au sehemu yeyote ambayo mtu hawezi kuigusa na usubiri hadi siku ya Jumatano ambapo utaiandika baadhi ya maneno.

Mambo ya muhimu kukumbuka hapa ni kwamba;

Lazima fito au fimbo hiyo ikatwe na itengenezwe katika siku na saa za sayari ya Shams yaani siku ya Jumapili mnamo

·        saa 1:00 – 1:59     (saa moja asubuhi) au
·        saa 8:00 – 8:59     (saa nane mchana) au
·        saa 3:00 – 3:59     (saa tatu usiku) au
·        saa 10:00 – 10:59          (saa kumi usiku).

Ni bora zaidi iwapo tendo la kuikata hii fimbo maalumu likifanyika mnamo alfajiri siku ya Jumapili wakati jua linachomoza.

Iwapo itashindikana saa hizo basi ikate katika siku na saa za sayari ya Shams kama ilivyoelezwa hapo juu.

Alama za kuandikwa kwenye fimbo hii zinatakiwa ziandikwe katika siku na saa za sayari Attwarid (Mercury) yaani siku ya Jumatano mnamo.

·        saa 1:00 – 1:59     (saa moja asubuhi) au
·        saa 8:00 – 8:59     (saa nane mchana) au
·        saa 3:00 – 3:59     (saa tatu usiku) au
·        saa 10:00 – 10:59          (saa kumi usiku).

Alama za kuandikwa katika hii fimbo ni




Alama nyingine ni


Alama hizi zote mbili zinatakiwa ziandikwe kwa damu ya Njiwa na inabidi kiandikio (Kalamu ya kuandikia) iwe ni Nyoya refu la bawa la kulia la Bata bukini (goose) au ukikosa kabisa tumia nyoya la Bata Mzinga au Bata wa kawaida.

Maneno yafuatayo ni lazima yatamkwe baada ya tendo la kuandika katika hiyo fimbo litakapokamilika.

Sema;

“Kwa nguvu za ADONAI Mkuu ninaiamuru hii fimbo iweze kufanya kazi ambazo mimi ninataka inifanyie bila ya kupungua uwezo wowote ule. Iwe na nguvu kubwa za kunilinda na kuvuta kwangu na kunifanikisha kile ninachotaka kukifanya kwa amri za ADONAI na kwa nguvu za radi za Mkuu Zariatnatmik, conjuro te cito mihi obedire”

Hiyo fimbo inatakiwa uinuize na uifukize kwa mafusho yanayotakiwa kisha ihifadhiwe katika kitambaa cha Hariri.

Iwapo ukikosa kitambaa cha Hariri basi tafuta kitambaa chochote safi, chekundu ambacho hakijawahi kutumiwa.

N.B:

Fimbo hii maalum baada ya kutayarishwa namna hii inaweza kutumika mara kwa mara katika kipindi cha mwaka mmoja (1) tokea ikatwe na kutengenezwa kwa mara ya kwanza, bila ya kuhitajika kutengenezwa fimbo nyingine.




NYOYA LA BATA BUKINI (GOOSE):

Nyoya maalum la Bata Bukini ni kifaa cha kingine ambacho kina umuhimu wa kipekee katika shughuli ya kuita Jini.

Nyoya linalohitajika hapa ni lile la Bata Bukini Dume.

Nyoya hili maalum ni lazima litayarishwe katika siku ya Jumatano katika saa yoyote ingawa ni bora zaidi ikiwa aidha saa 1 au 8 mchana.

Ni lazima litayarishwe kulingana na maelezo yake. Ni muhimu nyoya hili liwe linatoka katika bawa la kulia la Bata Bukini.

Iwapo utakosa hilo nyoya la bawa la kulia la Bata bukini (goose) unaweza ukatumia nyoya la Bata Mzinga au Bata wa kawaida awe Dume na, bora tu nyoya hili liwe linatoka katika bawa la kulia la huyo Bata.

Pamoja na kazi nyingine nyoya hili hutumika katika kuandikia maneno maalum wakati wa matayarisho na wakati wa kumuita Jini.

Jinsi ya kulitayarisha:

Jinsi ya kutayarisha nyoya la bawa la upande wa kulia la bata mzinga ni kama ifuatavyo;

Nyofoa nyoya la tatu (3) kutoka upande wa kulia wa bawa la kulia la bata mzinga dume mnamo siku ya Jumatano.

Wakati ukinyofoa hilo nyoya sema maneno yafuatayo;

“ABRACHAY, ABATOY, SAMATOY, SCAVER, ADONAI, fukuza na uondoe kutoka katika hili nyoya nguvu zote zenye pingamizi ili hili nyoya liwe na nguvu zote zinazohitajika ili niweze kuandika chochote ninachotaka kuandikia na nifanikiwe”

Baada ya kulipata hilo nyoya, lichukue na ulihifadhi katika kitambaa cha hariri alafu ulihifadhi sehemu ambayo halitaweza kuonekana na mtu ili likae hapo hadi usiku siku hiyo au nyingine yeyote ya Jumatano.

Itakapofika usiku wa Jumatano mnamo saa 3 au 10 utoe ule unyoya wa bata mzinga ulioutayarisha alafu uufukizie mafusho mazuri yanayonukia.
Wakati unafukiza hayo mafusho kwenye hilo nyoya, sema maneno yafuatayo:

Sema;

“Ninataka huu unyoya ufanye kazi yake inayotakiwa katika kuandikia mambo ambayo nitauamuru bila ya shida yeyote, kwa Nguvu za ANSTON, CERRETON, STIMULATOR, ADONAY ambazo nguvu zake ni kubwa juu ya kitu chochote”

Huo unyoya ni lazima ufukizwe kwa mafusho kwanza kabla ya kuanza kufanyiwa kazi siku yake itakapofika.


KITAMBAA CHA HARIRI

Kitambaa cha hariri ni kifaa cha kingine ambacho kina umuhimu wa kipekee katika shughuli ya kuita Jini.

Kitambaa cha hariri kinachohitajika hapa ni kile kisafi na ambacho bado hakijatumika, na itakuwa vizuri kama kikipatikana ambacho hakijaguswa guswa na watu.

Kitambaa hiki cha hariri ni lazima kinunuliwe au kitayarishwe katika siku ya Jumatano katika saa yoyote ingawa ni bora zaidi ikiwa aidha saa 1 au 8 mchana.

Ni lazima kitambaa hiki kitayarishwe kulingana na maelezo yake.

Kitambaa hiki kinatakiwa KISIWE cha rangi nyeusi au Kahawia (brown).

Pamoja na kazi nyingine, kitambaa hiki hutumika katika kuhifadhi baadhi ya vitu vitakavyotumika wakati wa kabla na baada ya kumuita Jini.

Iwapo itakuwa shida kupatikana kwa hiki kitambaa cha hariri basi unaweza ukatumia kitambaa chochote safi laini na ambacho hakijatumika kabisa ni hii ni muhimu sana.

Baada ya kupata hicho kitambaa cha hariri mnamo siku hiyo ya Jumatano mnamo saa 3 au 10 usiku kufukize mafusho yanayonukia vizuri sana.




Wakati ukiwa unafukiza mafusho haya sema maneno yafuatayo;

Sema;

“Ninataka hiki kitambaa kifanye kazi yake inayotakiwa katika kuhifadhia vitu ambavyo nitaviweka bila ya shida yeyote, kwa Nguvu za ANSTON, CERRETON, STIMULATOR, ADONAY ambazo nguvu zake ni kubwa juu ya kitu chochote”

Baada ya kumaliza kukifukiza hiki kitambaa cha hariri kwa mafusho yanayonukia sana, kihifadhi sehemu nzuri ambayo hakiwezi kuguswa na mtu yeyote na kama tayari umeishatayarisha baadhi ya vifaa kwa ajili ya shughuli ya kumuita jini basi unaweza ukaviweka katika hiki kitambaa cha hariri.


NJIWA (DAMU YA NJIWA)

Damu ya njiwa ina umuhimu wa kipekee katika shughuli ya kuita Jini.

Njiwa ni lazima anunuliwe au atayarishwe katika siku ya Jumatano katika saa yoyote ingawa ni bora zaidi ikiwa aidha saa 1 au 8 mchana.

Damu ya njiwa katika shughuli hii ya

Njiwa wanatakiwa angalau wawili (2), yaani mmoja damu yake itatumika kwa ajili ya kuandikia

·        Fimbo maalum
·        Kitambaa cha hariri.

Wakati yule Njiwa wa pili Damu yake itatumika wakati wa kumuita jini.

Wanatakiwa wanunuliwe siku ya Jumatano, na itakuwa ni bora zaidi iwapo watanunuliwa mnamo saa 1 au 8 mchana, (yaani katika siku na saa ya sayari ya Attwarid - Mercury).



MAFUSHO

Mafusho yanayohitajika kwa ajili ya shughuli hii ni pamoja na yale yanayotokana na:

1.     Mshubiri (aloes).
2.     Basibasi (mace).
3.     Benzoin.
4.     Storax
5.     Ubani.

Pamoja na hayo, mafusho mengine yanayoweza kutumika ni yale ambayo yanayotoa harufu nzuri sana.


KWA KIFUPI:

Kwa ujumla siku na jinsi ambavyo baadhi ya vifaa vinavyotumika katika maandalizi ya kumuita jini ni kama ifuatavyo;

Kukata fimbo maaalum           ................... Jumapili.
Kupata unyoya                       ................... Jumatano
Kuufukiza unyoya                            .................... Jumatano
Kuandika kwenye Fimbo        ................... Jumatano
Kununua kitambaa cha hariri ................... Jumatano.
Kununua njiwa                        .................... Jumatano.



KUITA MAJINI

Kwa ujumla kuna nyakati mbili ambazo mtu anaweza kuwaita Majini wakatokea kirahisi zaidi.

Kwanza ni kwa kupitia saa za Sayari ya Atwarid (Mercury) kama jinsi ilivyoelezwa hapo juu.

Pili ni kwa kupitia ishara za mwezi; kulingana na kuandama, kupevuka au kufifia kwake, ingawa hata njia hii bado ni vizuri zaidi kama ikifanyika siku ya Jumatano, yaani wakati wa saa na siku za sayari ya Mercury (Atwarid)

Iwapo kama utaona inakuwa shida kujua muda wa kumuita Jini, Basi unaweza ukafanya wakati ambapo utaona mwezi umepevuka kabisa.

Unaweza pia ukafanya wakati mwezi ukiwa unaandama (hilali au mwezi kongo) huku ukiwa unatoa mwanga. Na huo ni wakati mzuri zaidi kwa kuandika maandishi yeyote yale ambayo yanahitajika kwa kufanya shughuli hiyo.

Hata hivyo inatakiwa iwe ni siku ya Jumatano (yaani siku ya sayari ya Mercury) na saa ziwe ni zile za Mercury (yaani aidha saa 3 au 10 usiku).

5 comments:

  1. Alama za kuandika kwenye fimbo mboa hazipo

    ReplyDelete
  2. Naitwa Dr. LUSAJO Kama unataka utajiri kwa muda mfupi ukiwa na nia masharti ni ya kawaida kutokana na uwezo niliopewa na Mwenyezi mungu maisha yako yanabadilika ndani ya muda mfupi kikubwa ni wewe kufuata masharti kwa umakini mzuri. wasiliana nami kwa namba hizi +255 754082579 TAFADHARI PIGA SIMU HUSITUME SMS

    ReplyDelete
  3. Nashukuru sana Sheik kukusoma ndani ya blog Yako. Ila sikittiko kuhusu fimbo ya angerani, haukutupa maandishi ya kuweka juu yake.

    ReplyDelete