Vipindi za kila siku

[habari][bleft]

MAWE

[mawe][bleft]

NYOTA

[nyota][twocolumns]

videos

[videos][bleft]

MAJINI

[majini][twocolumns]

About Me

My photo
I am an Astrologer, Politician,,Jounalist by proffession,very much interested in current affairs and political news around the world.

SIRI ZA MILIMA YA SAYARI KATIKA VIGANJA.



SIRI ZA MILIMA YA SAYARI KATIKA VIGANJA.

Milima ya Viganja ni Sehemu Moja muhimu sana katika Usomaji wa Mikono. Milima hii inawakilisha Sayari husika ambayo Inatawala maeneo hayo.

Milima hii kwa ujumla inapatikana sehemu mbalimbali katika Kiganja ambapo mingi ipo sehemu za chini za baadhi ya Vidole. Milima hiyo ya Sayari pamoja na sehemu iliyopo ni kama ifuatavyo;

1.    Mlima wa Zuhura {Mount of Venus}:

Mlima huu wa Sayari ya Zuhura (Venus) ni Sehemu iliyoinuka katika Mkono chini ya Kidole Gumba.

Tafsiri za Mlima huu ni kama ifuatavyo;

·        Iwapo Mlima huu utakuwa ni Mkubwa, Mgumu na wa Duara; Inaashiria Mtu huyo atakuwa Mwenye Afya Njema, Mwenye Roho nzuri, Mkweli, Mwaminifu, Mpole, Mwenye Huruma na Anayewapenda Watoto

·        Iwapo Mlima huu utakuwa Bapa na Haujainuka juu; Inaashiria Mtu huyo ana tabia ya kujitenga na watu, mwenye afya isiyoridhisha, mwenye tabia ya kufanya mambo yake peke yake na mwenye kujizuia kutenda baadi ya mambo.

·        Iwapo Ukiwa Mkubwa, Inaashiria Mtu huyo ana Maisha Marefu.

·        Ukiwa Mkubwa, Mrefu kuliko kawaida, Inaashiria Mtu huyo ana Nguvu sana za kufanya mambo na Anapenda maisha ya Anasa sana kwani kwake yeye anaona Anasa kama ni kitu muhimu sana Maishani.

·        Ukiwa Mgumu na Mrefu; Inaashiria Mtu huyo anapenda sana kufanya Mapenzi.

·        Ukiwa Mrefu na Mlaini; Inaashiria Mtu huyo ana tabia ya Kubadilika badilika na Ana Ashiki na Tamaa nyingi.

·        Iwapo Sehemu ya Chini ya Mlima huu wa Zuhura Imechomoza zaidi kuliko sehemu nyingine Inaashiria Mtu huyo anatumia Nguvu zaidi kwenye Mambo ya Usanii na Sanaa.

2.    Mlima wa Chini wa Sayari ya Mariikh (Mars):

Mlima huu wa Chini wa Sayari ya Mariikh (Mars) ni Sehemu ya Katikati ya Kidole cha Shahada na Kidole Gumba ... pale panapotengeneza “Alama ya V” baina ya Vidole hivi viwili.

Tafsiri za Mlima huu ni kama ifuatavyo;

·        Iwapo Mlima huu utakuwa ni wa Saizi ya kawaida Inaashiria Mtu huyo ana Nguvu, Akili nzuri na Ana uwezo wa Kutulia wakati wa matatizo na Shida.

·        Iwapo Mlima huu utakuwa Bapa, na Haujanyanyuka Juu; Inaashiria Mtu huyo ni Mwoga na Anayeogopa Shida.

·        Iwapo Mlima huu utakuwa Mkubwa sana; Inaashiria Mtu huyo ni Mgomvi, Kuna uwezekano pia akawa na Roho mbaya na ya Ukatili, Mbishi na ambaye Haogopi kufanya Mambo ya Hatari.

3.    Mlima wa Sayari ya Mushtara (Jupiter):

Mlima huu wa Sayari ya Mushtara (Jupiter) ni Sehemu ya Chini ya Kidole cha Shahada..

Tafsiri za Mlima huu ni kama ifuatavyo;

·        Iwapo Mlima Huu utakuwa ni wa Saizi ya Kawaida, Inaashiria Mtu huyo ana Msukumo wa Kutegemea mambo mazuri, Malengo Mazuri, Roho Nzuri na Rafiki kwa Ujumla.

Pia Mtu huyo anajiamini, ni Mkarimu ingawa Anapenda Kujivuna, Ufahari na Mambo ya Kidini.

·        Iwapo utakuwa Bapa na Haujanyanyuka Juu; Inaashiria Mtu huyo ni Mchoyo, Bahili, Mvivu, Asiyejiamini na wala Hajali Hisia za Wengine.

·        Iwapo Mlima huu wa Mushtara ni Mkubwa sana na umepanda Juu Sana Inaashiria Mhusika huyo anapenda Kujisifu, Makuu, Kiburi na Kujigamba. Inaashiria ya Kuwa Mtu Mtu anajali Malengo yake peke yake.

·        Iwapo Mlima Huu Unaungana na Mlima wa Zohal (Saturn... yaani Sehemu ya Chini ya Kidole cha Kati); Inaashiria Mtu huyo Atapata Furaha na Faida zaidi Iwapo atafanya Kazi kwa Ushirikiano na Mtu mwingine kuliko Kufanya Yeye Mwenyewe.

4.    Mlima wa Sayari ya Zohal (Saturn):

Mlima huu wa Sayari ya Zohal (Saturn) ni Sehemu ya Chini ya Kidole cha Kati.

Tafsiri za Mlima huu ni kama ifuatavyo;

·        Iwapo Mlima huu utakuwa ni wa Saizi ya Kawaida, Inaashiria Mtu huyo anapenda Kujichunguza Mafanikio yake, ni mtu Madhubuti anayefikiria Juu ya Mambo muhimu, mwenye kupenda Kujielimisha (Kusoma), Mwenye Busara na Anayejiwekea Akiba ya Baadae.

·        Iwapo Mlima huu utakuwa Bapa na ambao haujajitengeneza vizuri; Inaashiria Mtu mwenye Bahati kubwa.

·        Iwapo Mlima huu wa Sayari ya Zohal ni Mkubwa sana na Umepanda Juu sana, Inaashiria Mtu huyo ni Mwenye Huzuni, Kusikitika, Kusononeka, Anaejitenga na wenzake, Mwenye Kuwaza mambo mabaya ya Kutisha na Anayeweza hata Kujiua.

·        Iwapo Mlima huu unaegemea kwenye Mlima wa Sayari ya Mushtara (Jupiter)... yaani chini ya Kidole cha Shahada; , Inaashiria Mtu makini Mwenye Malengo makubwa.

·        Iwapo Mlima huu unaegemea kwenye Mlima wa Sayari ya Shams (Jua)... yaani chini ya kidole cha pete; Inaashiria Mtu huyo anapenda sana vitu na mambo mazuri.


5.    Mlima wa Sayari ya Shams (Sun):

Mlima huu wa Sayari ya Shams (Sun) ni Sehemu ya Chini ya Kidole cha Pete... yaani Kidole cha Pili kutoka Kidogo.

Tafsiri za Mlima huu ni kama ifuatavyo;

·        Iwapo Mlima huu una Saizi ya Kawaida; Inaashiria Mtu anayefurahisha, Mwenye Roho nzuri, Mwenye Bahati na mwenye uwezo mkubwa wa kazi za Sanaa.

·        Iwapo Mlima huu ni Bapa na Haujajengeka vizuri, Inaashiria Mtu asiyechangamsha, asiyekuwa na malengo yanayoeleweka ya maisha, asiyevutiwa wala kupenda aina yeyote ya kazi za Sanaa wala Utamaduni.

·        Iwapo Mlima huu utakuwa ni Mkubwa sana na Umepanda Juu sana; Inaashiria Mtu huyo anapenda Kujidai, Mlaghai, Mbadhirifu, Mwenye Madoido mengi na mwenye kupenda Anasa.

·        Iwapo Mlima huu wa Sayari ya Shams unaegemea Mlima wa Sayari ya Attwarid (Mercury)... yaani chini ya Kidole kidogo, Inaashiria Mtu huyo ana uwezo Mkubwa wa Kupata Pesa nyingi kwa kufanya Kazi za Usanii au Sanaa.

·        Iwapo Mlima huu umeungana na Mlima wa Sayari ya Attwarid (Mercury); Inaashiria Mambo yote yanayojionyesha katika kidole kidogo kiutabiri yatakuwa hivyo hivyo.


6.    Mlima wa Sayari ya Attwarid (Mercury):

Mlima huu wa Sayari ya Attwarid (Mercury) ni Sehemu ya Chini ya Kidole Kidogo.

Tafsiri za Mlima huu ni kama ifuatavyo;

·        Iwapo Mlima huu una Saizi ya Kawaida; Inaashiria Mtu huyo ana Uwezo wa Kufikiria kwa Haraka sana Ingawa ni Vigumu Kumuelewa, Mwerevu, Aliyechangamka, Mwenye uwezo mkubwa wa kushawishi watu, Mchapakazi, Anayependa mambo ya aina mbalimbali.

·        Iwapo Mlima huu wa Sayari ya Attwarid utakuwa Bapa na ambao Haujajitengeneza Vizuri; Inaashiria Kutochangamka, Kutokuwa na Malengo Maishani, Kudanganywa; yaani Kwa kifupi Inawakilisha kushindwa maishani.

·        Iwapo Mlima huu utakuwa ni Mkubwa; Inaashiria Mtu huyo atakuwa na Utashi Mzuri.

·        Iwapo Mlima huu utakuwa ni Mkubwa sana na Uliopanda Juu sana; Inaashiria Mtu huyo ni Tapeli mwenye Uwezo Mkubwa wa Kuwadanganya watu, pia Anayependa Vitu na Mali.

·        Iwapo Mlima huu utakuwa una Mistari Mifupi Mifupi iliyokatiza juu yake; Inaashiria Mtu huyo ana Kipaji kikubwa cha Kuponya watu, Pia inamaanisha Upendo. Aina hii ya Mlima huu huwa upo kwenye Viganja vya Madaktari na Manesi wengi.

7.    Mlima wa Juu wa Sayari ya Mariikh (Mars):

Mlima huu wa Juu wa Sayari ya Mariikh (Mars) ni Sehemu ya Kati kati kwa Pembeni ya Kiganja... yaani Chini zaidi ya Kidole kidogo pale Kiganja kinapojikunjia.

Tafsiri za Mlima huu ni kama ifuatavyo;

·        Iwapo Mlima huu una Saizi ya Kawaida; Inaashiria Mtu huyo ana Moyo wa Ujasiri

·        Iwapo Mlima huu wa Juu wa Sayari ya Mariikh (Mars) utakuwa Bapa na ambao Haujajitengeneza Vizuri; Inaashiria Mtu Mwoga anayejifikiria Yeye tu.

·        Iwapo Mlima huu utakuwa Mkubwa sana na Umenyanyuka Juu sana; Inaashiria Mtu mwenye Hasira, Anayependa Kukejeli na Mwenye akili ya Kutenda maovu.


8.    Mlima wa Sayari ya Qamar (Moon):

Mlima huu wa Sayari ya Qamar (Moon) ni Sehemu ya Chini ya kabisa usawa wa Kidole Kidogo kwenye Kona ya Kiganja.

Tafsiri za Mlima huu ni kama ifuatavyo;

·        Iwapo Mlima huu una Saizi ya Kawaida; Inaashiria Mtu Mwenye uwezo mkubwa wa Kuhisi na Kutambua Jambo litakalotokea, Mbunifu, Mwenye Fikra Nyingi, Mwenye Kipaji cha Sanaa na Mwenye Mapenzi Makubwa na Bahari.

·        Iwapo Mlima huu wa Juu wa Sayari ya Qamar (Moon) utakuwa Bapa na ambao Haujajitengeneza Vizuri; Inaashiria Mtu asiye Mbunifu, Asiye na Huruma, Asiye Imara na ni Mtu anaeng’ang’ania Msimamo wake.

·        Iwapo Mlima huu utakuwa Mkubwa sana na Umenyanyuka Juu sana; Inaashiria Mtu Mwenye Fikra za kupita kiasi, mwenye Kujipima na Kuna uwezekano asiwe Mkweli katika Mambo yake.

·        Iwapo Mlima huu wa Juu wa Sayari ya Qamar (Moon) utakuwa Mrefu na Imara (Mgumu); Inaashiria Mtu Mbunifu na Mwenye uwezo Mkubwa wa Kutoa Mawazo bora.

·        Iwapo Mlima huu wa Juu wa Sayari ya Qamar (Moon) utakuwa Mrefu na Mlaini, Inaashiria Mtu Mwenye mawazo yanayobadilika badilika na Mwenye Hisia za Kushuku.

·        Iwapo Mlima huu wa Juu wa Sayari ya Qamar (Moon) utakuwa Unafika Kwenye Mlima wa Sayari ya Zuhura (Venus)... yaani kwenye Mlima uliopo chini ya Kidole Gumba; Inaashiria Mtu mwenye Mapenzi Makali.

·        Iwapo Mlima huu wa Juu wa Sayari ya Qamar (Moon) utakuwa Unafika kwenye Kifundo cha Mkono; Inaashiria Mtu mwenye Nguvu za Mizungu na Siri (Occult Powers).



SIRI ZA VIGANJA

MILIMA YA SAYARI ZA KWENYE VIGANJA














 

No comments: