MAJINI WAASI part II
MAJINI WAASI part II
Mfalme Suleiman
alikuwa Mfalme wa binadamu na Majini yote. Wakati wa enzi yake kuna baadhi ya
Majini waliokuwa wakikataa kutii amri zake hivyo alikuwa akiwaadhibu..
Kuna Majini 72
ambao waliasi kabisa na Mfalme Suleiman aliamua kuwafunga kabisa ili wasiwepo
kabisa miongoni mwa binadamu. Majini hao aliwakamata na kuwafungia katika
Gudulia la Shaba na kuwatumbukiza katika Ziwa.
Karne nyingi baada
ya kuondoka Mfalme Suleiman watu wa Babiloni waliokuwa wakitafuta hazina
waliliona Gudulia hilo na wakalivunja wakidhani kuna mali hivyo kuwapa uhuru
majini hao ambao walirudi katika sehemu zao walizokuwa zamani.
Majina na kazi za
Majini hao ni kama ifuatavyo:-
1.
BAAL:
Yeye ni Mfalme anayetawala
Mashariki ana uwezo wa kukufanya usionekane na kukupa busara. Akikutokea huwa
na kichwa cha binadamu, Chura au Paka na wakati mwingine huweza kukutokea kwa
sura zote tatu kwa pamoja. Huzungumza kwa sauti nzito kama farasi.
2.
AGARES.
Yeye ni Mtawala anaetawala
Mashariki, hujitokeza kama mtu Mzee aliyekaa juu ya Mamba akiwa ameshika fimbo
kwenye mkono wake. Yeye anauwezo
wakuwafanya wanaokimbia wasimame, kuwarudisha wale waliokimbia, anafundisha
lugha zote, anaharibu sifa zote za kidini na husababisha mitetemeko ya ardhi.
3.
AMON. Yeye ni mwanajeshi mzalendo na mwenye nguvu,
hutokea kama mbwa mwitu mwenye kichwa cha nyoka na akitema ndimi za moto na
huweza kubadilika katika umbo la binadamu pale anapoamrishwa na mwenye kumwita
lakini huwa na meno kama ya mbwa. Ana uwezo wa kutoa habari zilizopita na za
baadae, huleta mapenzi na kupatanisha marafiki na maadui.
4.
BARBATOS. Yeye ni Lodi (Lord) na Mtawala, hutokea
wakati jua linapokuwa kwenye Nyota ya Mshale na huja akiwa amezungukwa na wafalme wanne na askari
watatu. Ana uwezo wa kutoa ushauri katika masuala yote ya sayansi, hugundua
hazina zilizofichwa kwa uchawi au mazingaombwe, anajua yaliyopita na yajayo.
Hupatanisha marafiki na wale wenye madaraka.
5.
PAIMON. Yeye ni mfalme mkuu mwenye utiifu kwa
LUCIFER, hutokea kama mtu aliyevikwa taji amekaa juu ya ngamia mwenye nundu
moja, akiwa amezungukwa na wanamuziki. Anazungumza kwa sauti ya kuunguruma.
Anafundisha sanaa, sayansi na siri. Hutoa na kudhibitisha heshima na kuwafanya
watu wawe ni wenye kutumika kwa matakwa ya wachawi na hukupa umashuhuri.
6.
BUER. Yeye ni Rais ambaye hutokea wakati jua linapokuwa kwenye Nyota ya Mshale na
hufundisha falsafa, mantiki na maadili ya miti shamba na hutibu magonjwa yote
na hukupa umashuhuri.
No comments: