Vipindi za kila siku

[habari][bleft]

MAWE

[mawe][bleft]

NYOTA

[nyota][twocolumns]

videos

[videos][bleft]

MAJINI

[majini][twocolumns]

About Me

My photo
I am an Astrologer, Politician,,Jounalist by proffession,very much interested in current affairs and political news around the world.

Mawe ya kila nyota



Mawe ya kila nyota

 

MAWE YAPUNDA

Aventurine

"Mponyaji wa Roho na Moyo." Linaleta katika usawa nguvu za kiume na za kike, ubunifu,  uongozi na furaha. Pia linasaidia katika kufikia maamuzi sahihi. 
Jiwe hili lina uwezo wa kumfunika mvaaji katika blanketi la mapenzi.
Linakinga na kusaidia katika uponyaji wa magonjwa ya moyo, mapafu na adrenalini.  

Bloodstone

Hili ni jiwe linaloleta nia na uwezo wa kufanikiwa, maisha marefu, nguvu ya mfano wa fimbo ya chuma pia linauwezo wa kuondoa ugumu wowote katika njia ya kutaka kufanikiwa.
Linaleta uaminifu na heshima katika uhusiano, kulirudisha tena penzi pamoja na kufuta madoa na vidonda vya penzi. Linampeleka mtumiaji katika maisha mazuri ya kimapenzi.
Linasaidia kutibu matatizo ya damu, mapafu, macho na moyo.

Carnelian

Malengo thabiti na msukumo. Jiwe hili linasaidia kuleta kwa mtumiaji kujiamini na ujasiri. Linahamashisha,linaanzisha uwezo binafsi na kuonyesha na kuamsha vipawa vilivyojificha vya mtumiaji.
Linauwezo wa kumlinda mvaaji dhidi ya mambo yote yasiyo mazuri na kutokujiamini.
Linasaidia kujikinga na kutibu Asthma (Pumu) na Shinikizo la damu.

Citrine

"Jiwe la utajiri" linafungua na kuunganisha uwezo wa mtumiaji na uwezo wa kupata mafanikio katika alifanyalo ili kupata utajiri.
Ubunifu na uanzishaji, kudhibiti akili ili iweze kufikiria kwa mapana na marefu jambo linalotakiwa kufanyika ili liweze kufanikiwa. Pia huweza kudhibiti na kuongoza mawazo ili yawe yanawaza kufanikiwa katika mambo mbalimbali. 
Linasaidia usagaji wa chakula katika mwili na mzunguko wa damu. 
Diamond  (Almasi)
"Mfalme wa mawe yote". Jiwe hili linawakilisha nguvu za kudra unadhifu na nguvu. Linatokana na madini ya Carbon ambayo ndiyo chanzo cha maisha yote. Jiwe hili linamsaidia mvaaji kujigeuza na kuwa mtu mkamilifu bora zaidi. 
Jiwe hili linawakilisha alama ya kuaminiwa, kujihusisha kikamilifu uaminifu (Maumbile yetu ya kweli) na mapenzi. Almasi (diamonds) yamekuwa yakijulikana kuwa na mvuto wa matamanio, kipaji na wingi wa mali.
Husawazisha umetaboli (hali ya ujenzi na uvunjaji wa kemikali mwilini) na kusafisha mwili dhidi ya sumu na kukuza uwezo wa macho kuona.
Lapis Lazuli (Nili na zali)
Hili ni jiwe la "kurahisisha kipaji cha kutambua mambo". Lilitumiwa na Wamisri wa zamani kama kinga ya kuingia sehemu takatifu.
Lina uwezo wa kutakasa mwili na akili na kuondoa uchafu wote unaosababishwa na Mashetani na Mizimu. Vilevile linakufanya uwe na uhusiano mzuri na watu na unazipa nguvu sehemu zako za kinga ya mwili.
Mexican lace agate  
Kuamsha nguvu za mwili. Lina uwezo wa kurudisha nguvu za mwili wakati unapojihisi kukosa nguvu ya kufanya baadhi ya mambo . Linafichua ukweli  wa mambo (siri) na lina uwezo wa kumfanya mvaaji aweze kufahamu juu ya undani wa maisha na jinsi ya kuyashinda.
Linasaidia kutibu ngozi, moyo, uti wa mgongo na meno.
Quartz
Jiwe hili linakuza uwezo wa kutunza, malengo,kujirekebisha, kuhifadhi na na nguvu za kimwili na kiroho. 
Linakuza uwezo wa kuhisi jambo kabla halijatokea. Pia lina uwezo wa kumfundisha mtumiaji  kwa kadri ya uwezo wao na kasi zao. Vile vile linampa mtumiaji uwezo mkubwa wa mambo mbalimbali.
Hematite
"Jiwe linalotawala akili." Linamuwezesha mtu kukumbuka kitu vile kilivyo, uhakika, kusawazisha, na utulivu wa akili. Linaondoa matatizo au mambo yaliyo kinyume na kuyabadilisha na kuyafanya  kuwa upendo.
Jiwe hili vile vile linaleta mapenzi, na uhusiano wa amani. 
Pia linasaidia kuponya upungufu wa damu na uvimbe katika kichwa. 

MAWE YA NG’OMBE
Emerald (Zumaridi)
Huleta usalama katika mapenzi. Linamuwezesha mvaaji kuingia na kujua siri zilizo ndani kabisa ya moyo kwa hivyo kuponya na kuamsha matamanio ya juu kabisa ya mioyo yetu. Ni la nguvu lenye uwezo wa kukuwezesha kuona yalioyo ndani na kubashiri yajao.
Jiwe hili linasaidia kuponya ugonjwa wa macho na kigugumizi. Jiwe hili linautuliza moyo na akili na kukufanya kuwa mwenye kujiamini.
Kyanite
Jiwe hili ni "daraja kati ya akili na maudhui". Ni kito chenye nguvu ya kukupa ufunuo na mwamko au hamasa. Linamfanya mvaaji awe katika hali nzuri kwa wale wanao penda kufanya Taamuli (meditation). Vile vile linatibu matezi madog madogo.  
Chrysocolla
"Jiwe la kutibu la Mama Ardhi" Jiwe hili ni la tiba na linachangamsha akili na linapoza hasira na kukupa amani ya ndani ya mwili na nguvu. Jiwe hili linavutia mafanikio na linaleta bahati nzuri. Linauwezo vile vile wa kuondoa fikra mbaya na kuweka akili yako wazi katika kufanya mambo. Linauwezo wa kutibu ugonjwa wa sukari, pumu na ugonjwa wa damu(Leukemia) 
Diamond(Almasi)
"Mfalme wa mawe yote". Jiwe hili linawakilisha nguvu za kudra unadhifu na nguvu. Linatokana na madini ya Carbon ambayo ndiyo chanzo cha maisha yote. Jiwe hili linamsaidia mvaaji kujigeuza na kuwa mtu mkamilifu bora zaidi. 
Jiwe hili linawakilisha alama ya kuaminiwa, kujihusisha kikamilifu uaminifu (Maumbile yetu ya kweli) na mapenzi. Almasi (diamonds) yamekuwa yakijulikana kuwa na mvuto wa matamanio, kipaji na wingi wa mali.
Husawazisha umetaboli (hali ya ujenzi na uvunjaji wa kemikali mwilini) na kusafisha mwili dhidi ya sumu na kukuza uwezo wa macho kuona.
Rose Quartz
"Jiwe la uchangamfu na mapenzi" Jiwe linatibu maumivu ya hisia. Linaupa moyo uchangamfu wa kupenda vitu vizuri. Lina kulinda na kuondoa hasira na hisia mbaya. 
Rhodonite
"Jiwe la mapenzi ya kindugu". Jiwe hili linauwezo wa kufanya ujiamini na kujituma. Kichwa, moyo na mwili huunganishwa na jiwe hili na kuku fanya wewe mvaaji upate hamu ya kufanya mambo yako. Linatibu maradhi ya moyo mapafu. koo na viungo.
Kunzite
"Jiwe la Umoja"  Jiwe lianunganisha moyo, kichwa na koo na linakuwezesha kuwa na hisia za mapenzi, ufahamu na uwezo wa kujieleza. Linauwezo wa kuusafisha mwili na vile vile linakuwezesha kuzungumza mbele za watu na uhuru wa ndani ya mwili na pia linatibu Moyo. 
Selenite
"Jiwe la mchawi" Jiwe hili linauwezo wakukupa wewe mvaaji uwezo wa kujua matatizo ya mtu na kumtibu. Linasaidia na kusafisha uti wa mgongo na kutibu maradhi ya kigeugeu, vile vile linatibu magonjwa yasiyotibika.
Hematite
"Jiwe linalo tawala akili." Linamuwezesha mtu kukumbuka kitu vile kilivyo, uhakika, kusawazisha, na utulivu wa akili. Linaondoa matatizo au mambo yaliyo kinyume na kuyabadilisha na kuyafanya kuwa upendo.
Jiwe hili vile vile linaleta mapenzi, na uhusiano wa amani. 
Pia linasaidia kuponya upungufu wa damu na uvimbe katika kichwa.
MAWE YA MAPACHA
Celestite
Hili ni jiwe la "Mapenzi ya malaika", linaleta amani ndani ya mwili, matumaini na mtazamo mzuri. Lina uwezo wa kukupa uwezo wa juu katika uzungumzaji na mawasiliano.
Linasaidia kuona vizuri, kusikia na linatibu maradhi yeyota ya akili.
Howlite

Jiwe la utulivu wa moyo, mawazo na hisia nzuri. Linamuwezesha mtumiaji awe mwaminifu, mkweli na mwenye uwezo wa kuongea vizuri na kwa uwazi.
Linaondoa woga na hasira. Linampa mtumiaji utambuzi, subira, kuwa na malengo na matarajio ya kuwa kila kitu na mambo yote yatakuwa mazuri.
Chrysocolla

"Jiwe la kutibu la Mama Ardhi" Jiwe hili ni la tiba na linachangamsha akili na linapoza hasira na kukupa amani ya ndani ya mwili na nguvu. Jiwe hili linavutia mafanikio na linaleta bahati nzuri. Linauwezo vile vile wa kuondoa fikra mbaya na kuweka akili yako wazi katika kufanya mambo. Linauwezo wa kutibu ugonjwa wa sukari, pumu na ugonjwa wa damu (Leukemia)
Emerald  (Zumaridi)
Huleta usalama katika mapenzi. Linamuwezesha mvaaji kuingia na kujua siri zilizo ndani kabisa ya moyo kwa hivyo kuponya na amsha matamanio ya juu kabisa ya nyoyo zetu. Ni la nguvu lenye uwezo wa kukuwezesha kuona yalioyo ndani na kubashiri yajao.
Jiwe hili linasaidia  kuponya ugonjwa wa macho na kigugumizi. jiwe linautuliza moyo na akili  na kukufanya kuwa mwenye kujiamini.

MAWE YA KAA
Moonstone
Hili ni jiwe la kuomba utakacho na kikawa kweli, maono na hukufanya uwe katika hali nzuri kimawazo. Linaleta mambo yote uyatakayo, mwanzo mpya, kuzaliwa upya. Linaleta upendo na msaada mkubwa kama ule anaokupatia Mama. 
Linaondoa maumivu na magonjwa. Linauwezo wa kutengeneza mirija na viungo vya mwili vilivyoharibika kutokana na magonjwa pamoja nakutibu njia za uzazi.
Peacock Ore  
Hili ni jiwe la furaha, uzima, uchangamfu na linaleta matumaini na nguvu za kutenda. Linasaidia kuleta mawazo mazuri ya kipekee kabisa ambayo yanakufanya uweze kuchukua mwelekeo mwingine mzuri ambao utakupa matumaini, kujiamini na kufanikiwa pamoja na kuaminiwa.
Linamlinda mtumiaji dhidi ya mawazo ya kutokufanikiwa, linauwezo wa kutibu mfumo wa fahamu, mapafu na moyo.


MAWE YA SIMBA
Petrified Wood
Jiwe hili lina uwezo wa kumfanya mtumiaji aweze kujua mambo yote ya maisha yaliyopita wakati wa taamuli (meditation) kama likitumika kwa ajili hiyo. Linamletea mtumiaji utulivu na ushwari wa moyo, usawa, uthabiti, afya njema na maisha marefu.
Linaleta ulinzi dhidi ya magonjwa na linasaidia kuponya mifupa, kuufanya imara uti wa mgongo na matatizo ya kusikia.
Garnet
Jiwe la kujitoa kwa ajili ya watu wengine, binafsi na katika malengo ya binafsi. Linaamsha "moto wa ndani" wa ubunifu. Linatoa ufufuo wa usawa kwa mtumiaji. Linahamasisha mapenzi na hisia kali za kimapenzi.
Jiwe hili linavuta bahati nzuri, ulinzi dhidi ya uchafu wenye sumu. Linakinga dhidi ya huzuni, mfadhaiko, upungufu wa damu na matatizo mbalimbali ya mwili.
Jasper  
"Jiwe kuu lenye jukumu kubwa la mafunzo na malezi". Linathaminiwa sana na Washamen kama jiwe takatifu na lenye nguvu linalotoa ulinzi na uthabiti. Linatoa ulinzi wakati wa safari za kinyota.
Linavuta nguvu za jua zenye uwezo wa kuufanya mwili kurudia hali ya ujana na kuupa nguvu. Linasaidia kuzalisha upya seli za mwilini (tisu) na mfumo wa harufu. 
Onyx 
Jiwe hili lina uwezo wa kumfanya mtu kujitawala mwenyewe. Linaleta kwa mtumiaji uwezo wa kufahamu mambo mbalimbali, ulinzi wakati wa Taamuli na ndoto. Linafichua uwezo wa ndani wa mtu uliojificha.
Linasaidia sana katika kutibu glakoma (ugonjwa unaotanua mboni ya jicho na kutatiza kuona), kifafa na uharibifu wa seli.


MAWE YA MASHUKE
Cuprite
Jiwe hili linauwezo wa kumpatia mtumiaji nguvu kubwa ya uhai na kuipitisha moja kwa moja mpaka kwenye maeneo yanayohitaji kujengwa upya na kurudishiwa uhai kamili pamoja na kutengeneza mfumo mzima wa uhai.
Linaleta ufahamu na kujielewa katika mwili pia linasaidia kuponya magonjwa yasiyotibika na yasiyokuwa na dawa.
Sugilite
"Jiwe la Mapenzi ya juu kabisa". Lina nguvu ya kutibu na kukufunza njia za kujitibu mwenyewe katika mpangilio wa mambo yako.
Lina uwezo wa kukufanya ukumbuke mambo na uwe na uwezo wa ndani wa kiroho wa kujieleza mbele za watu.
Jiwe hili linatibu maradhi ya kichwa na kansa.
Moss Agate
Jiwe hili humpatia mtumiaji usawa na kujiamini pamoja na wingi wa vitu. Linaleta mpangilio mzuri na uzuri. Linatia mkazo hadhi nzuri ya mtumiaji. Ni jiwe zuri kwa wakulima na watu wanaojishughulisha na mambo ya ardhi.
Linasaidia kutibu mzio (allergy), na matatizo ya ngozi.
Peridot
Ni jiwe zuri la urafiki na furaha. Linatia afya na nguvu mwili mzima. Linavipa na kuviimarisha viungo vya mwili na kuhamasisha kukua vizuri kwa mwili. 
Linaleta usawa katika mfumo wa maisha. Linamlinda mtumiaji dhidi ya mambo yote ambayo si mazuri.
Linasaidia katika kutibu maradhi mbalimbali yakiwemo vidonda vya tumbo, tezi dundumio na koromeo.
MAWE YA MIZANI
Lepidolite
Hili linaitwa "Jiwe Bibi". Jiwe hili linakupumzisha na linakupoza na linamtuliza mvaaji kutokana na matatizo na fikra mbaya.
Lina uwezo wa kuifanya akili ipambanue njia sahihi za kufanya mambo na marekebisho na linamsaidia mvaaji kupambanua mapitio ya hisia zake za kuzaliwa, kufa na kuzaliwa tena.Jiwe hili linaponya misuli iliyovimba na uchovu.
Rose Quartz
"Jiwe la uchangamfu na mapenzi" Jiwe linatibu maumivu ya hisia. Linaupa moyo uchangamfu wa kupenda vitu vizuri. Lina kulinda a kuondoa hasira na hisia mbaya. 
Opal 
Hili ni jiwe linalomuwezesha mtu kupata maono mbalimbali. Linaongeza nguvu za kujua mambo kabla hayajatokea. Lina uwezo wa kumuonyesha mtumiaji mambo mengi yaliyojificha katika nafsi za watu, linavuta nguvu za utambuzi, na ubashiri.
Hili jiwe la Opal linamfunika mtumiaji kwa usiri, mambo ya siri na haiba kubwa. Jiwe hili lina uwezo wa kumsaidia mtumiaji kutoweka na kutokuonekana anapoamua kufanya hivyo.
Linatibu maambukizo mbalimbali, linaponya na kuwezesha macho kuona zaidi pia linasaidia katika kazi za umetaboli (uwezo wa mwili kusaga chakula)
Prehnite  
"Jiwe la kupaa", linasaidia mtumiaji katika safari za kiroho na kinyota. Linalinda na kukuza nguvu ya maisha. Linasaidia kuwasiliana na Malaika na viumbe wengine wa Mbinguni. Linakuza uwezo wa kujua mambo kwa undani sana pamoja na utabiri.
Linasaidia kutibu ugojwa wa upungufu wa damu, figo na jongo (gout).
MAWE YA N’GE
Ruby
"Malkia wa mawe yote". Jiwe la mapenzi, linamzungushia mtumiaji hali ya uzuri na lina uwezo mkubwa wa kubadilisha muonekano wa mtu.
Linamlinda mtumiaji dhidi ya mambo yote mabaya, kuumia na maradhi. Linavuta uimara, uthabiti, kuimarika, uaminifu, utiifu na uwajibikaji. Inaaminiwa kuwa kama hili jiwe litakuwa ni la duara basi utajiri ni lazima utaupata.
Jiwe la Ruby linatoa mtikisiko wa joto linaloponya; na kwa mujibu wa habari za kale, iliaminiwa kuwa jiwe hili linauwezo wa kutoa joto(moto) lekundu ambalo lina uwezo wa hata kuchemsha maji, ambalo lina uwezo wa kugeuza na kubadili moto wa mapenzi.
Jiwe hili linasaidia kuponya moyo, uchafu wote katika damu na kuondoa sumu mwilini.
Rhodochrosite
Jiwe hili linaitwa "Mwalimu wa Kimalaika wa mapenzi na usawa", linaunganisha na kuleta uwiano kwa mume na mke na lina uwezo wa kukuvutia mpenzi wa uhakika kwa yule anayelivaa na kukupa uwezo wa namna ya kupenda.
Jiwe hili linahamasisha mapenzi ya kujipenda wewe mwenyewe na dunia kwa ujumla.
Kunzite  
"Jiwe la Umoja" Jiwe lianunganisha moyo, kichwa na koo na linakuwezesha kuwa na hisia za mapenzi, ufahamu na uwezo wa kujieleza. Linauwezo wa kuusafisha mwili na vile vile linakuwezesha kuzungumza mbele za watu na uhuru wa ndani ya mwili na pia linatibu Moyo.


Selenite
"Jiwe la mchawi" Jiwe hili linauwezo wakukupa wewe mvaaji uwezo wa kujua matatizo ya mtu na kumtibu. Linasaidia na kusafisha uti wa mgongo na kutibu maradhi ya kigeugeu, vile vile linatibu magonjwa yasiyotibika.
Moldavite
"Mponyaji kutoka ulimwengu mwingine" Linauwezo wa kumuwezesha mtumiaji kuwasiliana na Falme za juu mbinguni. Linatoa nuru na mwanga katika mawasiliano na mbingu nyingine.
Linamtayarisha mtumiaji kwa ajili ya kujibadilisha kwa ajili ya kupaa katika mbingu nyingine. Lina uwezo wa wa kupitisha nuru maalum ambayo inataka kufanana na miale ya leza (Laser beam) ambayo ina uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa mbalimbali.
Opal 
Hili ni jiwe linalomuwezesha mtu kupata maono mbalimbali. Linaongeza nguvu za kujua mambo kabla hayajatokea. Lina uwezo wa kumuonyesha mtumiaji mambo mengi yaliyojificha katika nafsi za watu, linavuta nguvu za utambuzi, na ubashiri.
Hili jiwe la Opal linamfunika mtumiaji kwa usiri, mambo ya siri na haiba kubwa. Jiwe hili lina uwezo wa kumsaidia mtumiaji kutoweka na kutokuonekana anapoamua kufanya hivyo.
Linatibu maambukizo mbalimbali, linaponya na kuwezesha macho kuona zaidi pia linasaidia katika kazi za umetaboli (uwezo wa mwili kusaga chakula)
Unakite
Tiba ya kibinafsi. Jiwe hili linasawazisha hisia na linatumainisha Pendo Kuu.
Linatayarisha na kusaidia katika namna ya kuzaliwa upya na katika namna halisi ya kuzaliwa kwani jiwe hili lina uwezo wa kuchangamsha tiba ya njia ya uzazi na lina uwezo wa kufichua sababu za maradhi.
Topaz 
"Jiwe la jua" linasaidia mtumiaji kuwaza na kutimiza ndoto zake. Jiwe hili linatoa joto na mwanga wenye nguvu za kisumaku za kuponya, kuondoa wasiwasi na mashaka, maumivu na maradhi.
Lina uwezo wa kuvuta mapenzi na mafanikio pia kuwasiliana na milki nyinginezo.
Linasaidia kuvunja kuganda kwa nguvu za mwili na katika kuondoa uchafu wa sumu katika mwili.

MAWE YA MSHALE
Turquoise (Feruzi)
"Jiwe linalounganisha mbingu na ardhi". Linaunganisha nguvu za Milki au Ufalme katika ngazi ya juu kabisa.
Linatengeneza njia ya elimu na ufahamu kwa anayelivaa kwa sababu ya utukufu wake. Jiwe hili vilevile linamlinda na kumbariki mvaaji na hutuliza akili na mwili.
Lapis Lazuli
Hili ni jiwe la "kurahisisha kipaji cha kutambua mambo". Lilitumiwa na Wamisri wa zamani kama kinga ya kuingia sehemu Takatifu.
Lina uwezo wa kutakasa mwili na akili na kuondoa uchafu wote unaosababishwa na Mashetani na Mizimu. Vilevile linakufanya uwe na uhusiano mzuri na watu na unazipa nguvu sehemu zako za kinga ya mwili.
Azurite
"Taa katika giza". Inaangaza katika giza la akili. Jiwe hili linauwezo wa kusafisha, kufanya upya, kuamsha fahamu na kuanzisha "akili za kimbingu" duniani.
Jiwe hili linauwezo wa kuanzisha nguvu ya kuona. Linasaidia kuponya koo, bandama na uti wa mgongo.
Amber 
"Dhihirisho". Jiwe la bahati nzuri, linaleta nguvu ya utakaso, nguvu za jua na kufyonza nguvu ya dunia na kutengeneza nguvu thabiti kwa mtumiaji. 
Jiwe hili lina uwezo wa kutoa maradhi mwilini na kuuweka mwili katika hali nzuri. Linasafisha maudhi.


Cookeite
"Mganga wa Waganga". Hili ni jiwe la tiba. Lina uwezo wa kutuliza, kupoza na kusafisha dhamira mbaya na mawazo machafu.
Jiwe hili linahamasisha ushirikiano na kukufanya uwe na moyo mwepesi. Jiwe hili lina mvuto wa Malaika.
Opal 
Hili ni jiwe linalomuwezesha mtu kupata maono mbalimbali. Linaongeza nguvu za kujua mambo kabla hayajatokea. Lina uwezo wa kumuonyesha mtumiaji mambo mengi yaliyojificha katika nafsi za watu, linavuta nguvu za utambuzi, na ubashiri.
Hili jiwe la Opal linamfunika mtumiaji kwa usiri, mambo ya siri na haiba kubwa. Jiwe hili lina uwezo wa kumsaidia mtumiaji kutoweka na kutokuonekana anapoamua kufanya hivyo.
Linatibu maambukizo mbalimbali, linaponya na kuwezesha macho kuona zaidi pia linasaidia katika kazi za umetaboli (uwezo wa mwili kusaga chakula)
Selenite
"Jiwe la mchawi" Jiwe hili lina uwezo wa kukupa wewe mvaaji uwezo wa kujua matatizo ya mtu na kumtibu. Linasaidia na kusafisha uti wa mgongo na kutibu maradhi ya kigeugeu. Vile vile linatibu magonjwa yasiyotibika.
Unakite  
Tiba ya kibinafsi. Jiwe hili linasawazisha hisia na linatumainisha Pendo Kuu.
Linatayarisha na kusaidia katika namna ya kuzaliwa upya na katika namna halisi ya kuzaliwa kwani jiwe hili lina uwezo wa kuchangamsha tiba ya njia ya uzazi na lina uwezo wa kufichua sababu za maradhi.


Topaz 
"Jiwe la jua" linasaidia mtumiaji kuwaza na kutimiza ndoto zake. Jiwe hili linatoa joto na mwanga wenye nguvu za kisumaku za kuponya, kuondoa wasiwasi na mashaka, maumivu na maradhi.
Lina uwezo wa kuvuta mapenzi na mafanikio pia kuwasiliana na milki nyinginezo.
Linasaidia kuvunja kuganda kwa nguvu za mwili na katika kuondoa uchafu wa sumu katika mwili.
Herkimer Diamond
"Jiwe la ndoto" lina uwezo wa kufichua ukweli wa ndoto. Linampatia mtumiaji uwezo wa kujua mambo kabla hayajatokea. Pia lina uwezo wa kupeleka ujumbe wa upendo na uponyaji kwa mtu aliyembali (sehemu nyingine).
Jiwe hili linalinda dhidi ya mnururisho na linaondoa sumu mwilini.
MAWE YA MBUZI
Tiger eye  
Jiwe hili lina uwezo wa kutengeneza hali nzuri sehemu ambayo kuna machafuko. Linaleta amani na maelewano, kusawazisha hisia, huleta hali ya kuwa makini na uthabiti kwa mtumiaji. 
Inaboresha hisia za nafsi na uwezo wa kutambua mambo, linavuta urembo, uzuri, wingi wa vitu na hekima. 
Jiwe hili linasaidia kuponya vidonda, michubuko, macho na koo.
Malachite
"Kubadilisha". Mponyaji mwenye nguvu, jiwe hili lina uwezo wa kuondoa maradhi moja kwa moja. Linasafisha na kuonyesha njia ya wazi ya kufanya mambo. Linasaidia katika kufanya mambo ambayo moyo unayataka ili yawe ya kweli na yatokee.
Jiwe hili la Malachite lina uwezo wa kuupa nguvu mwili wa kujua mambo bila kuambiwa na kujua chanzo cha tatizo. Linalinda dhidi ya mnunurisho. 
Garnet
Jiwe la kujitoa kwa ajili ya watu wengine, binafsi na katika malengo ya binafsi. Linaamsha "moto wa ndani" wa ubunifu. Linatoa ufufuo wa usawa kwa mtumiaji. Linahamasisha mapenzi na hisia kali za kimapenzi.
Jiwe hili linavuta bahati nzuri, ulinzi dhidi ya uchafu wenye sumu. Linakinga dhidi ya huzuni, mfadhaiko, upungufu wa damu na matatizo mbalimbali ya mwili.
MAWE YANDOO
Cookeite
"Mganga wa Waganga". Hili ni jiwe la tiba. Lina uwezo wa kutuliza, kupoza na kusafisha dhamira mbaya na mawazo machafu.
Jiwe hili linahamasisha ushirikiano na kukufanya uwe na moyo mwepesi. Jiwe hili lina mvuto wa Malaika.
Staurolite
"Jiwe la bahati nzuri, moyo wa ushujaa na ulinzi. Linampa mtumiaji usalama. Linasaidia katika kumfanya mtu ajielewe kwa undani kabisa na lengo lake la kuwa hapa duniani, na kulitekeleza. 
Jiwe hili linamuunganisha mtumiaji na ulimwengu wa kinyota.
Boji stone
Jiwe hili linasafisha na kuipa nguvu nyota ya mtumiaji. Linatoa nguvu ambayo inapita vizuizi vyote, huku ikileta usawa na kutibu mwili na akili.
Jiwe hili linafungua milango ya kuwasiliana na viumbe wengine pamoja na kuzaliwa upya na utambuzi wa mambo yaliyowahi kutokea kabla na ambayo yatatokea baadae. 


MAWE YA SAMAKI
Blue Lace Agate
Jiwe hili linaongeza kasi ya kiroho na imani ya dini, na kukupa msukumo wa mambo. Linasafisha mparaganyo katika akili na roho pia linaondoa mfadhaiko.
Linatibu ugojwa wa baridi yabisi na kuumwa na kichwa.
Flourite
"Jiwe la utambuzi" linasafisha ukungu wa mawazo ya uongo. Linatengeneza amani na utulivu katika ghasia. Linaleta umakini, afya njema, usafi katika kila kiwango kwenye mwili na amani. 
Linasaidia katika kutibu maradhi ya kuambukiza na  uvimbe.
    


    
    




3 comments:

  1. Mm nimezaliwa taerehe 22/02/ naomba utabiri wangu

    ReplyDelete
  2. Mm nimezaliwa taerehe 22/02/ naomba utabiri wangu

    ReplyDelete
  3. Asalaam aleykm mm nyot yangu ni mshale na mke wangu ni mashuke inawezekana kufanya kitu ili ziendane maana teyari nina watoto 4 na ya mate ya pete yapo kumi je kila jiwe linakuwa kweye tofauti au yanakuwa kwenye pete moja na ni sh ngapi

    ReplyDelete