NGUVU ZA MAWE
QUARTZ:
Mawe aina ya Quartz ni mawe muhimu sana kwa
binaadamu katika maisha ya kila siku.
Mawe haya hutumika kwa kutengenza miwani ya kusomea, Darubini na Vingamuzi
Mwanasayansi ajulikanae kwa jina la Marcel Vogel ambae
ni mchunguzi wa mambo ya kisayansi katika kampuni ijulikanayo kama IBM kwa
miaka ishirini na saba, na ndiye aliyekua na madaraka ya kutumia madini ya aina
ya PHOSPHORS kwa kutengeneza TV za rangi, (Phosphors ni aina ya madini ambayo
hutoa mwanga kwa kupata joto), alisema kwamba vituo vyote vya kurushia
matangazo hutumia mawe au madini kama njia kuu ya mawasiliano. Kipande cha jiwe
la aina ya Quartz (Silicon Dioxide) hukatwa kwa namna maalum na kutegeshwa
mpaka kutoa masafa( frequencies) yatakikanayo.
Saa za aina ya Quartz zimepata majina yao kutokana
na madini au mawe ya aina ya Quartz. Madini hayo yanatumika kwa sababu ya
uhakika wa kuweka muda sawa.
Vile vile Bwana Frank Dorland ambaye jina lake
linaheshimika sana katika mambo ya madini, hasa kwa kuyakata katika miundo maalum.
Mbeleni alikuwa ni msanii maarufu katika sanaa za kidini na mwenye kuhifadhi
vitu vihusianvyo na usanii. Aliazimwa jiwe la aina ya Quartz lilochongwa kwa
mfano wa fuvu la mtu maarufu ajulikanae kama Mitchelle Hedges.
Anasema walipokua wakiweka mikono yao juu ya jiwe
hilo walihisi kama vile kutekenywa na nguvu au moto wa umeme, waliona vivuli
vikitembea ndani yake, walisikia sauti na nyimbo na hata wakati mwingine walihisi
harufu ya marashi ya aina ya Apple-Blossom. Hapo ndipo alipoelewa jiwe hilo lilitengenezwa
kufanya mazingaumbwe kwa kutumia mwanga.
Katika mwaka wa 1980 Bwana Dael Walker ambae ni
mkurugenzi wa Taasisi ya Utambulisho wa Mawe ya Marekani alikodi kibanda katika
maonyesho ya Jimbo la New York ya Marekani ili kufanya utafiti kuhusu mawe na
nguvu zake za uponyaji.
Kati ya watu 234 ambao walijaribiwa kwa kupunguza
maumivu waliyokua nayo kwa kushika jiwe,
227 katiyao walithibitisha mafanikio makubwa waliyoyapata kwa kupungukiwa na
maumivu yaliyokuwa ya kiwasumbua au kuisha kabisa.
Mawe huingiana na fikra na hisia na vile vile
hushirikiana na akili. Huongeza nguvu za fikra na hisia hivyo kupunguza maumivu,
kusononeka na vile vile humuwezesha mutu kupona kwa haraka.
MOONSTONE: Ni jiwe lenye rangi nyeupe
maji maji, nalo husaidia kujenga hisia na kusisimua mapenzi hasa
wanapobadilishana jiwe hilo kati ya
wapenzi wawili, na vile vile hufungua moyo ili kutoa na kupokea mapenzi.
Jiwe hili la Moonstone huongeza uwezo wa kuwatunza
na kuwajali watu wengine.
DIAMOND (ALMASI) :
Hili ni jiwe la akili linaloashiria kudumu,
lisiloweza kugeuzwa au kushawishiwa na lenye nguvu zisizo onekana.
Diamond ni neno la kitaliani linalomaanisha mpenda
Mungu. Na mara nyingine hutumika kuota ndoto na kuwezesha kuona mbali
vizuri.Jiwe hili ni sasa, lakini vilevile ni jiwe la siku zijazo.
Kulingana na wanasayansi wa Kigiriki inasemekana
Eros Mungu wao wa mapenzi alikuwa akitumia mishale iliyokuwa imewekwa Almasi
kwenye ncha zake ili kuwahamasisha watu waingie katika mapenzi baina yao.
Vilevile inasemekana wanaume walikuwa wakinunua almasi
tatu katika maisha yao.
Almasi ya kwanza ilikuwa ni ya mke wake
wanapofunga ndoa, Almasi ya pili ilikuwa ya mpenzi wake wa nje ya ndoa na ya
tatu ilikuwa ya kumpa mke wake pindi anapogundua kuwa ana mpenzi mwingine.
No comments: